album mpya ya belle 9...isubili

Anaitwa Abednego
Damian aka Belle 9, msanii ambaye alianza mziki kitambo ila mwaka 2008
ndipo alipopata nafasi yakujulikana na watanzania pale alipotoka na
wimbo wake wa SUMU YA PENZI na mpaka kupelekea kutoka na album yake ya
kwanza aliyoipa jina la Sumu Ya Penzi.
Sasa hivi Belle 9
anaiandaa album yake mpya ambayo itakuwa ni album ya pili iliyopewa
jina la VITAMIN MUSIC. Mbali na album hiyo Belle 9 anatarajia kutoka na
Mixtape yake aliyoipa jina la NO RAPERS NO MC NO SINGER. Mbali na hivi
vyote anasema mashabiki wake watarajie ngoma mpya muda wowote baada ya
mwezi huu mtukufu.
0 comments: