Vijana walioathirika dawa za kulevya kusaidiwa
VIijana walioathirika na dawa za kulevya jijini Dr es Salaam watanufaika na mpya utakaowasaidia kuondokana na tatizo hilo.
Aidha, vijana hao watapata nafasi ya kushiriki kutoa video chini ya usimamizi wa kampuni binafsi ya OpenAir Media Communications, ambayo inatekeleza mradi huo utakaitwa Kuwapa Sauti Vijana Walio Katika Mazingira Hatarishi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mshirika wa OpenAir Media Communications, Pius John, alisema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kampuni hiyo kusaidia jitihada za serikali kuwaondoa katika tatizo hilo mamilioni ya watumiaji wa dawa za kulevya hasa vijana.
“Lengo letu kuu ni kuwasaidia watumiaji wa dawa ya kulevya kuondokana na tatizo lenyewe, kuwajengea tabia ya kujishinda na kubadilisha tabia kwa kuwashirikisha katika utengenezaji wa video,” alisema Pius John.
Alisema mradi huo wa mwaka mmoja unafadhiliwa na Tanzania Media Fund (TMF) na kwamba kampuni ya Medecins du Monde itasaidia katika mambo ya kitaalamu.
Katika utekelezaji wa mradi huo, John alisema Open Air Media itatoa mafunzo ya kina kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuhusu utoaji wa wa video, kuhariri, weledi wa kuchukua picha au matukio, uwasilishaji wa ujumbe, uwezeshaji na vitu vingine kupitia PVP.
Alisema hatua hiyo itawasaidia vijana hao kupata weledi unaotakiwa kutengeneza video katika masuala mbalimbali yahusuyo dawa za kulevya, afya na mambo mengine.
“Tunataka watumiaji wa dawa za kulevya kwanza waeleze masuala yanayowaathiri wenyewe yanayohusu dawa ya kulevya na utumiaji wake. Tunataka pia waweze kujadili masuala yanayowahusu na hivyo kuwasaidia namna ya kuwajibika katika jamii,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja Mshirika wa OpenAir Media Communications, Ken Bayona, alisema kuwa, mradi huo pia utawasidia vijana kupata jukwaa la kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa kushiriki na kuunda klabu, kutengeneza video na kuziuza katika maeneo yao.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: