Tozo la simu kujadiliwa bungeni latoweka
Tegemeo
la umma kwa serikali kuwasilisha bungeni muswada wa mabadiliko ya
sheria iliyoanzisha tozo la Shilingi 1,000 kwa mwezi kwa watumiaji wa
simu za kiganjani, limetoweka.
Hali hiyo inatokana na Bunge kupanga ratiba ya shughuli zake kwa Mkutano wa 12 unaoanza Jumanne wiki ijayo mjini Dodoma, pasipo kuwapo muswada wa mabadiliko ya Sheria ya fedha inayoanzisha tozo za simu.
Viongozi kwa nyakati tofauti wamekuwa wakinukuliwa wakisema kuwa suala hilo litarejeshwa Bungeni kujadiliwa upya baada ya kulalamikiwa na wananchi ambao wanapinga kodi hiyo mpya.
Hata hivyo, rasimu ya ratiba ya mkutano wa 12 wa bunge utakaoanza wiki ijayo, ambayo NIPASHE imeiona imeonyesha miswada itakayojadiliwa ni saba huku suala la kodi ya simu likiwa halijawekwa kabisa kujadiliwa katika mkutano huo.
Wakati wa mkutano wa bajeti la Bunge uliomalizika Juni mwaka huu, Bunge lilipitisha sheria ya fedha inayoanzisha kodi kwenye Kadi ya simu ambayo kila mtumiaji simu, bila kujali matumizi yake atakuwa analipa Sh. 1,000 kwa mwezi.
Baada ya kupitishwa kwa kodi hiyo ambayo pendekezo lake lilitolewa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa wakati anasoma hotuba yake ya Bajeti, utekelezaji wake ulipangwa kuanza Julai mosi, mwaka huu.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na NIPASHE jana alisema suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na Idara ya Hazina iliyopo Wizara ya Fedha.
“Tumeshakubaliana suala hili lishughulikiwe na Hazina, kwa hiyo halipo tena kwenye Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,”alisema Profesa Mbarawa.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Dk. Mgimwa alipoulizwa alisisitiza kuwa uamuzi wa kurejesha suala hilo bungeni upo pale pale hata kama rasimu ya ratiba ya mkutano wa 12 imeshatolewa.
“Kilichofikiwa hivi sasa ni kulifikisha suala hilo bungeni, katika mkutano utakaoanza wiki ijayo,”alisema Dk.Mgimwa.
Waziri huyo alipoulizwa kama uamuzi wa serikali ni huo kwanini suala hilo halijapangwa kujadiliwa katika mkutano wa 12 unaoanza wiki ijayo, alisema utaratibu uliopo ni kwamba kabla ya bunge kuanza vikao vyake Kamati ya Uongozi ya Bunge hukaa kujadili mambo ya kujadiliwa bungeni.
Wakati msimamo wa serikali kuhusu suala hilo ukiwa hivyo, rasimu ya ratiba ya mkutano wa 12 wa bunge iliyotolewa na Kamati ya Uongozi ya Bunge, imeonyesha pamoja na mambo mengi miswada itakayojadiliwa ni saba kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu bunge hilo litakapoahirishwa.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa muswada wa sheria ya Tiafa ya umwagiliaji ya mwaka 2013 itajadiliwa, ukifuatiwa na muswada wa sheria ya takwimu wa mwaka 2013 utakaojadiliwa Agosti 29 mwaka huu.

Septemba 2, mwaka huu wabunge watajadili muswada wa sheria ya vyama vya ushirika wa mwaka 2013 na Septemba 4 mwaka huu, muswada wa sheria ya mfuko wa Akiba wa GEPF wa mafao ya wastaafu wa mwaka 2013.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wabunge watapata fursa ya kujadili muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013 Septemba 9 mwaka huu na mwisho watajadili muswada wa sheria ya kura ya maoni wa mwaka huu 2013.
Kutokana na ratiba hiyo, ni wazi kuwa suala la tozo la kodi za simu halitajadiliwa hali ambayo itaacha maswali mengi kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia suala hilo litawaumiza watu wenye kipato kidogo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Ruvuma Julai 21, mwaka huu alisema tozo hilo si ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza umeme vijijini na kwamba wanaopinga hawatutakii mema.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: