ROONEY ANAWEZA KUFIKIRIA KUJIUNGA NA ASERNAL, LAKINI KAMA DILI LA CHELSEA LITAGONGA MWAMBA!!
Mshambuliaji
wa Manchester ambaye kwa sasa hajatulia klabuni hapo, baba wa watoto
wawili, Wayne Mark Roonye huenda akafirikiria kwenda washika bunduki wa
kaskazini mwa London, klabu ya Asernal endao ndoto yake ya kufanya kazi
na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho haitatimia.
Manchester
United wanakataa kumuuza Rooney kwa wapinzani wao wakubwa wa kuwania
ubingwa msimu ujao, lakini bado nyota huyo anataka kuondoka Old
Trafford.
Ingawa
Chelsea ni chuguo la kwanza kwa Rooney, mshambuliaji huyo raia wa
England anaweza kwenda Arsenal endapo David Moyes na bodi ya timu hiyo
watakataa ofa ya pili ya Jose Mourinho.
Anaondoka? Wayne Rooney anawindwa na klabu za Arsenal na Chelsea
Arsenal
walianza harakati za kumtaka Roonye ambaye atafikisha miaka 28 mwaka
huu wakati ule amepigwa benchi na Sir Alex Ferguson katika mechi muhimu
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi machi mwaka
huu.
Arsenal
wameonesha kuwa wanaweza kumlipa Rooney mshahara mzuri. Kwa sasa nyota
huyo analipwa pauni milioni mbili na elfu arobaini kwa wiki na
amebakisha miaka miwili katika mkataba wake, lakini The Gunners
watavunja rekodi ya klabu kwa kumlipa pauni lakini mbili kwa wiki na
mkataba wa miaka mitano.
Lakini
Chelsea bado wanaongoza mbio za kumsainisha Roonye baada ya kutuma ofa
ya pauni milioni 23, na kuongeza2.5 wiki iliyopita.
Baada
ya kupata majeruhi ya nyama za paja katika ziara yao ya maandalizi ya
msimu mpya wa ligi kuu, Rooney anaendelea na mazoezi mepesi katika
uwanja wao wa Carrington, huku akiwa na matumani kuwa klabu hizo mbili
zitakubaliana juu ya yeye kuihama United.
Mama
watoto wa Rooney, Coleen anaonekana kukubaliana na mume wake na ameweka
wazi kuwa anapenda kuishi jijini London na watoto wao.
Ushindani: Jose Mourinho na Arsene Wenger wote wanamhitaji Rooney kutoka United
Ana presha kubwa? David Moyes anaweza kumpoteza moja kati ya majembe ya United
Rooney
alizungumza kwa njia ya simu na kocha Moyes pamoja na mkurugenzi mkuu
Ed Woodward baada ya kutokea tofauti kati yao juu ya umuhimu wake
klabuni hapo.
Chelsea wanajiandaa kuongeza mzigo ili kumnasa Rooney, na taarifa zilizopatikana ni kuwa wanaandaa pauni milioni 30.
Kama United watakaa kumuuza Chelsea, basi itakuwa habari njema kwa Asernal kabla ya kumalizika kwa muda wa dirisha la usajili.
0 comments: