TWITE CHINI YA UANGALIZI WA DOKTA
BEKI wa Yanga raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC),
Mbuyu Twite yupo chini ya uangalizi wa daktari bingwa, Gilbert Kigady wa
Hospitali ya Trana Senta iliyopo Masaki, Dar
es Salaam.Mchezaji huyo yupo chini ya uangalizi
kutokana na uvimbe aliokuwa nao katika paja lake, baada ya kuumia wakati
akiitumikia timu hiyo
. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
Dar es Salaam
jana daktari wa Yanga, Nasoro Matuzia alisema bado hawajajua ni lini mchezaji
huyo ataanza mazoezi."Kwa sasa tunaona maendeleo yake
si mabaya tangu alipoanza matibabu kwa Dkt. Kigady, ila hatuwezi kusema lini
ataanza kuitumikia timu," alisema Matuzia.
Aliongeza kuwa wanafanya jitihada za
kumpatia matibabu mchezaji huyo kwa kuwa wanamtegemea katika kikosi cha Yanga.
0 comments: