Usichokijua kuhusu Nash MC na maisha ya msoto aliyoyapitia hadi sasa kuitegemea sanaa, awaasa Ma-MC wasikurupuke



Nash MC ni moja kati wa wasanii ambao mara nyingi wamekuwa wakitajwa na wasanii wenzao kuwa wanaijua na kuifuata misingi ya Hip Hop, hata Madee wa Tip Top aliyewahi kusema kwenye wimbo wake ‘Hip Hop ina misingi nyie wabongo hamuiwezi’, aliwahi kutamka kwenye kipindi cha power jam kuwa mwana hip hop pekee anaemkubali Tanzania kwa kufuata misingi ni Nash MC.

Anajulikana kama Maalim Nash, na hivi sasa anataka afahamike kama Nash MC Palestina, kupitia ukurasa wake wa Facebook alifunguka undani wa safari yake ya muziki, misoto aliyoipitia na watu waliomsaidia hadi kufika hapa alipo anaitegemea sanaa.
“Wakati namaliza kidato cha 4 mwaka 2003 pale benjamin william mkapa,matokeo yalipotoka sikubahatika kufaulu wala kuendelea na elimu ya juu,na baba yangu mzazi alikua tayari ashafariki tangu mwaka 1999,M.a.p baba yangu,na hali za familia zetu mtaani nadhani wengi mnazijua pale unapomaliza shule jinsi unavyochukuliwa pale nyumbani kwenu.utaanza kuambiwa uchangie hela za mboga,unga na majukumu yanaibuka ghafla tu,nilijiuliza maswali mengi sana hivi nitaishi vipi????
Sikua na kazi wala kibarua na sanaa haikua imestawi katika upande wangu,kwa kweli hali ilikua ngumu sana,ila mwenyezi Mungu hakunitupa mja wake alinikumbusha kua kuna kipaji amenipa na nachotakiwa ni kukifanyia kazi kwa juhudi na maarifa sana,nililiona hilo na nikaanza kuzama katika utamaduni wa hip hop kwa nguvu na akili zaidi kwa muda wa miaka mi 5 au 6 nikawa nasoma na kujifunza mambo mengi sana juu ya hip hop kiundani mno sikukurupuka kwenda studio na baada ya hapo nikaanza kuonekana zaidi katika matamasha ya wapi na hatimae siku 1 nikapewa kipindi na saigon katika kituo cha eatv,na kuelezea hip hop na misingi yake na itikadi pia watu wengi walianza kunipenda na kunikubali sana na miaka miwili mbele nikakutana na mjomba Zavara na Lindu hawa walinipa miongozo mikubwa sana katika safari yangu na na wimbo wa kwanza kurekodi ilikua chini ya mtayarishaji Kita pale rama records,ulikua unaitwa, ‘nani mkali kwenywe game’ lakini ikumbkwe kua mwaka 2000.

0 comments: