Watendji wabovu kucharazwa viboko

Diwani wa kata ya Busonzo wilayani Bukombe amewaagiza wananchi kuwakamata na kuwacharaza viboko watendaji na wenyeviti wa vitongoji wanaoshirikiana na matapeli kuwaibia watu wanaotuhumiwa kuwa wahamiaji haramu.



Diwani huyo, Charles Sahani, alitoa agizo hilo juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kitongoji cha Mkoni kijiji cha Nampalahala, wilayani Bukombe alipokuwa anajibu malalamiko ya baadhi ya wanakijiji.

Baadhi ya wananchi walihoji kuwa baadhi ya wenyeviti wa vitongoji, vijiji na watendaji wa vijiji kutoa vitisho wakiwashinikiza wananchi kutoa rushwa kati ya Sh. 200,000 hadi Shilingi milioni moja vinginevyo wafunge virago vyao licha ya kuwa raia halali.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

0 comments: