Bayern Munich kuwaacha hawa.

Mabingwa wa ulaya na bundesliga Bayern Munich wanakaribia
kuwauza wachezaji wake watatu ambao ni Diego Contento ,
Emre Can na Luis Gustavo Dias .
Wachezaji hao hawakupangwa kwenye mchezo wa jana (Jumatano)
kati ya Bayern Munich na Sao Paolo ambapo inaaminika kuwa
kocha Pep Guardiola amezungumza nao na kuwafahamisha kuwa
hawako kwenye mipango yake .
Emre Can na Diego Contento wamekuwa nje ya kikosi cha
kwanza na ilidhaniwa kuwa wangeondoka Bayern msimu
huu lakini kuondoka kwa Luis Gustavo kutawashangaza
wengi kutokana na mchango wake kwenye mafanikio ya
Bayern Msimu uliopita .
Nafasi ya Gustavo imekuwa finyu baada ya kusajiliwa kwa
wachezaji Mario Gotze na Thiago Alcantarra ambapo anajikuta
nje ya mipango ya kocha Pep Guardiola hali inayomfanya
alazimike kuondoka hasa katika kipindi hiki muhimu kabla ya
michuano ya kombe la dunia inayotaraji kufanyika nyumbani
kwao huko Brazil mwakani.
0 comments: