FAHAMU Award winning Video Director ambaye amehukumiwa miaka 90 jela kwa kuwabaka na kuwazalisha Binti zake
Mtayarishaji video
mwenye rekodi ya kushinda tuzo ambaye asili yake ni kutoka Naijeria,
Aswad Ayinde ambaye awali alikuwa amehukumiwa kwenda gerezani miaka 40
kwa kosa la kuwabaka binti zake, ameongezewa tena miaka mingine 50
katika kosa lake hili na kukamilisha jumla ya miaka 90 ambayo sasa
anapaswa kuitumikia.
Video producer huyu ambaye alikwishawahi kushinda tuzo ya MTV kwa kutengeneza video maarufu ya The Fugees - Killing Me Softly, amepewa hukumu hii nzito baada ya kukiri kosa mbele ya mahakama kuwa ni kweli alifanya uhalifu wa kuwabaka binti zake.
Ayinde ameeleza kuwa, alikuwa akifanya kitendo kama hiki mara kwa mara na lengo lake lilikuwa ni kuendeleza familia yake na damu yake kutengeneza kizazi chake ambacho kitadumu mpaka mwisho wa dunia.

Kitu cha kushangaza zaidi kutoka tukio hili ni kwamba Ayinde alifanikiwa kuwafanyia binti zake vitendo hivi, kuwapatia mimba na kuwazalisha mwenyewe ambapo aliweza kuitunza familia hii ambayo ilikuwa sasa na watoto sita kutoka miaka ya 80 mpaka mwaka 2002.
Ayinde alikuwa pia ana watoto wengine tisa kutoka kwa mke aliyekuwa ameachana naye, na watoto wengine watatu kutoka mama tofauti huko Brooklyn Marekani.
Ayinde amesomewa hukumu hii katika Mahakama huko New Jersey Marekani.

0 comments: