Hatma ya Ngassa kujulikana Agosti 13
Hatma
ya usajili wa mshambuliaji mpya wa Yanga, Mrisho Ngassa itajulikana
Agosti 13 baada ya kuibuka mgongano utokanao na jina la nyota huyo wa
timu ya taifa (Taifa Stars) kujitokeza pia katika orodha ya wachezaji
waliowasilishwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara.

Kwa nyakati tofauti, mahasimu wa jadi Simba na Yanga waliwasilisha jina la Ngassa kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kabla ya kufungwa kwa hatua ya kwanza ya dirisha la usajili na hivyo, kinachosubiriwa ni uamuzi wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kitakachofanyika jijini Dar es Salaam siku hiyo (Agosti 13) na kutoa maamuzi kuhusu mchezaji huyo na wengine watakaowekewa pingamizi.
Juzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuwasilisha usajili wao.
Yanga ilimtambulisha Ngassa kuwa ni mmoja wa wachezaji wake wapya itakaowatumia katika msimu ujao wa ligi utakaoanza Agosti 24 mwaka huu baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili huku mshambuliaji huyo akitangaza kuukana mkataba mwingine anaodaiwa kuwa aliusaini mwaka jana wakati akiichezea Simba.
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema kuwa wameamua kulipeleka jina la Ngassa kwa sababu ni mchezaji wao ambaye waliingia naye mkataba wa miaka miwili baada ya kutua kwao akitokea Azam.
Mtawala alisema kuwa wamepeleka jina la Ngassa kwa sababu wanaamini mshambuliaji huyo ni mali yao kufuatia mkataba aliosaini na kueleza kwamba mkataba huo walienda kuusajili pia katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
"Tumepeleka majina 29, la Ngassa ndani na kati ya hao wachezaji wa kigeni ni wanne," alisema Mtawala.
Aliongeza kuwa tayari klabu hiyo imejiandaa kupeleka pingamizi katika Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kwa sababu inajua jina la mchezaji huyo pia litakuwapo katika orodha ya wachezaji wa kikosi cha mahasimu wao wa jadi, Yanga.
Mtawala aliwataja wachezaji wa kigeni walioko kwenye orodha hiyo kuwa ni na Abel Dhaira, Joseph Owino wote kutoka Uganda, Amissi Tambwe na Gilbert Kaze wa Burundi.
Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa klabu yao imewasilisha majina ya wachezaji 28 wa kikosi cha kwanza na 18 wa timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20.
Kizuguto alisema kwamba anaamini katika fomu ya usajili itakayokuwa imewasilishwa na wapinzani wao Simba, haitakuwa imekamilika kama inavyotakiwa.
TFF jana ilitangaza kuongeza muda wa usajili kwa kuzitaka klabu kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika zoezi hilo.
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema jana kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu ili kupitia usajili huo, akieleza kwamba mwisho wa kuwasilisha pingamizi ni Agosti 12.
Hii si mara ya kwanza kwa mahasimu Simba na Yanga kumpigania mchezaji mmoja. Mwanzoni mwa msimu uliopita, uongozi wa Simba uliingia katika mgogoro na Yanga kuhusiana na usajili wa aliyekuwa beki wao, Kelvin Yondani.
Simba walidai kuwa Yondani ni mali yao, lakini mwishowe kamati iliyoshughulikia suala hilo ikasema kuwa inautambua mkataba aliosaini Yanga na hivyo 'Wekundu wa Msimbazi' wakaambulia patupu.
Mchezaji mwingine aliyegombewa na klabu hizo msimu uliopita ni Mbuyu Twite kutoka Rwanda ambaye hatimaye aliidhinishwa kuichezea Yanga baada ya kuonekana kuwa Simba haikufuata taratibu zinazotakiwa. Yanga waliamrishwa kuilipa Simba fedha walizokuwa wameshazilipa ili kumpata Twite.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: