Mfanyabiashara maarufu wa madini auawa Moshi
Mfanyabiashara
maarufu wa madini Jijini Arusha, Erasto Msuya, amepigwa risasi zaidi ya
10 katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (Kia) na kufa hapo hapo.
Msuya anayemiliki vitega uchumi lukuki Mkoani Arusha na Manyara, amepigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wakati akitokea Mererani katika migodi ya madini ya Tanzanite majira ya saa 6:30 mchana.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo kutoka uwanja wa ndege wa Kia, ambao hawakuwa tayari kutajwa majina yao, walisema mfanyabishara huyo baada ya kuuawa hakuna kitu chochote
kilichochukuliwa katika gari yake.
Hawa jamaa walimvizia njia panda ya Mererani na Kia na walivyofanikiwa kumsimamisha ghafla alitokea mtu, akiwa katika usafiri wa pikipiki na kummiminia risasi nyingi na alikufa hapo hapo,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Habari zaidi zilisema kuwa kwa sasa mamia ya wachimbaji wadogo wadogo wamesimamishwa kuchimba madini, kufutia tukio la mmoja wa wachimbaji wa kampuni ya Tanzanite One kupigwa risasi jambo lililoibua vita kubwa za kibiashara, kati ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi wameanza uchunguzi wa kina.
Kamanda Boaz alisema lilitokea njiapanda ya Mererani katika barabara kuu ya Moshi/Arusha.
Hata hivyo, Kamanda Boaz hakutoa taarifa za kina kwa maelezo kwamba alikuwa akielekea eneo la tukio.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwabaini wauaji na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: