`Wamachinga`watawala maonyesho ya Nanenane
Maonyesho
ya wakulima na wafugaji maarufu kama Nanenane, Kanda ya Mashariki
inayounda mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam yameonekana
kudorora kutokana na baadhi ya mabanda kukosa washariki.
Maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Dar es Salaam- Morogoro; na yalifunguliwa Agosti 01 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.
NIPASHE ilitembelea mabanda haya na kukuta idadi ndogo ya washiriki na pia wanaotembelea maonyesho ni wachache ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Baadhi ya mabanda yaliyofungwa ni la Wilaya ya Pangani mkoani Tanga kwa kile kichoelezwa kukosekana kwa fedha.
Mbali ya Halmashauri kutoshiriki, wizara mbalimbali nazo hazijashiriki kutokana na madeni.
Maonyesho hayo yametawaliwa na wafanyabiashara pamoja na wamachinga na baa.
Mwenyekiti wa chama cha wakulima kanda ya mashariki (Taso), Mohamed Mzee, alisema maonyesho hayo yamekuwa na idadi ndogo ya wananchi wanaotembelea kutokana na baadhi ya taasisi kutoshiriki.
Alisema Wizara za Kilimo, Chakula na Ushirika, Viwanda na Biashara pamoja na Mifugo na Uvuvi zinadaiwa zaidi ya Sh. milioni 56 na kwamba hiyo imechangia kukwamisha baadhi ya malengo ambayo kamati ilikuwa imejiwekea.

Alisema Taso inadai kiasi cha Sh. milioni 250 kutoka bodi, halmashauri na taasisi mbalimbali.
Mkoani Arusha, maonyesho hayo yametawaliwa na biashara za wamachinga badala ya wakulima.
NIPASHE ilitembelea maonyesho hayo katika viwanja vya Themi mjini hapa na kushuhudia wafanyabiashara wakinadi bidhaa zao badala ya wakulima kama inavyotakiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ibrahimu Msingi, alieleza kusikitishwa na wakulima wanaoshiriki maonyesho haya kwa maelezo kwamba wamekuwa wakihudhuria kwa mazoea.
Alisema nia ya maonyesho hayo ni kumkwamua mkulima na kwamba ni wajibu wao kuweka kumbukumbu pindi maonyesho yanapomalizika.
Aliitaka Taso Kanda ya Kaskazini kuwapa wafugaji kipaumbele na siyo shughuli za kibiashara.
Imeandikwa na Ashton Balaigwa, Morogoro na Woinde Shizza, Arusha

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: