Pengo: Tafuteni amani bila kutishia maisha ya wengine
Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp
Kardinali Pengo, amewaasa waumini wa kanisa hilo hapa nchini kuhakikisha
kwamba wanaitafuta amani pasipo kutishia maisha ya mtu mwingine yeyote
hata kama wao wanatishiwa.
Kardinali Pengo amesema amani inayotafutwa kwa kutishia maisha ya mtu mwingine kamwe haiwezi kuwa amani ya kweli.
Aliyasema hayo wakati wa Ibada Maalum ya Kipaimara iliyofayika katika Parokia ya Kimara jijini Dar es Salaam jana.
Kardinali Pengo alisema katika siku za hivi karibuni, kumekuwapo na hofu ya kutangaza Neno la Yesu Kristo kutokana na matishio dhidi ya imani yao, Kanisa na baadhi ya vifo kwa waumini wao wakiwa katika hali ya kutangaza Neno la Bwana.
"Nikijulikana kuwa namtangaza Yesu ni mwana wa Mungu, naweza nikauawa, kuchekwa ama nikapotezwa," alisema Kardinali Pengo mbele ya mamia ya waumini waliofurika katika ibada hiyo.

Aliongeza: "Pamoja na dharau na kashfa, lakini hatupaswi kurudi nyuma, ni jukumu letu kutangaza ukweli kuwa Yesu Kristo amefufuka, mwana wa Mungu na mkombozi wa dunia nzima."
Aliwataka waumini wa kanisa hilo nchini kutotishwa na kitu chochote ama mtu yeyote wanapomtangaza Yesu Kristo na kuwataka waendelee na ujasiri walionao.
"Papa Benedict XVI alituambia `tusiogope, tusihofu' na sasa Papa Francis XVI, anasema hivyo hivyo. Hakuna sababu ya kumfungia milango Yesu Kristo mkidhani mtakuwa salama. Ni kumfungulia tu milango," alisisitiza.
Kardinali Pengo alisema anatamani Yesu angekuja hapa nchini na kuwaeleza Watanzania `Amani iwe kwenu'.
"Na akishakuja na kuyasema hayo, nasi twende tukaitangaze kwa wengine," alisema.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: