soma majina ya wachezaji stars kuivaa Gambia............
Nyota
24 wakiwamo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa klabu ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameitwa kuunda kikosi cha timu ya
taifa (Taifa Stars) kitakachojiandaa kwa mechi ya kukamilisha ratiba ya
Kundi C la kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia dhidi ya
Gambia itakayochezwa Septemba 7, imefahamika.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jana kuwa wachezaji hao watatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 kabla ya saa 1:00 usiku na siku inayofuata wataanza mazoezi kujiandaa kwa mechi hiyo.
Wambura alisema kuwa kocha wa Stars, Kim Poulsen, ambaye hivi sasa yuko England akiongeza ujuzi kwa kujifunza katika klabu ya Swansea inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo, atarejea nchini Jumatatu (Agosti 26) kabla ya kuanza maandalizi ya mechi dhidi ya Gambia.
Aliwataja wachezaji walioitwa katika kikosi cha Stars kuwa ni makipa Juma Kaseja (huru), Mwadini Ali na Aishi Manula (wote Azam na Ally Mustafa 'Barthez' wa Yanga.
Mabeki ni Aggrey Morris na Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani, Nadir Haroub ' Cannavaro ' na David Luhende wa Yanga, Shomari Kapombe (Simba) na Vincent Barnabas (Mtibwa)
Viungo walioitwa kuitumikia Stars ni Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
Katika mechu yao ya kwanza iliyiochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda 2-1.
Ivory Coast wanaoundwa na nyota wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama Didier Drogba wa Galatasaray ya Uturuki na Yaya Toure wa Manchester City ya England wameshajihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya mtoano baada ya kuwa na uhakika wa kumaliza kileleni mwa Kundi C, wakizipiku Morocco, Stars na Gambia.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: