Tambwe: Nitaipa Simba ubingwa
Mfungaji
Bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la
Kagame), Mrundi Amissi Tambwe ameapa kujituma kwa uwezo wake wote na
kushirikiana na wenzake ili kuipa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara
klabu yake mpya ya Simba.

Akizungumza na NIPASHE kwenye hoteli aliyofikia iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana jioni, Tambwe alisema ametua Simba kuisaidia kupata mataji hasa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara ambao hivi sasa unashikiliwa na mahasimu wao wa jadi, Yanga.
“Kazi ya straika (mshambuliaji) ni kufunga. Nimekuja Tanzania kuisaidia Simba kufunga magoli. Naamini nitaendelea kufunga magoli mengi kama nitapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wachezaji wenzangu,” alisema Tambwe.
“Ligi ya Tanzania haitakuwa ngeni kwangu kwa sababu nawajua wachezaji wengi. Kina Cannavaro (Nadir Haroub), Yondani, Bocco… hawa wote nimekutana nao katika mechi za timu ya taifa,” aliongeza mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Burundi.
Kwa upande wake, beki Gilbert Kaze, ambaye alikuwa na Tambwe katika hoteli hiyo, alisema amefurahi kutua katika timu yenye mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania na kwamba, anaamini hali hiyo itamsaidia kuimarisha kipaji chake kutokana na ushindani uliopo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kulinganisha na kwao (Burundi).
“Ligi ya Tanzania ni ngumu na inahitaji nguvu. Mimi ni mgeni na ligi ya nchi hii lakini nawajua baadhi ya wachezaji kama Kaseja, Nyosso, Nyoni na Kavumbagu … nawajua vizuri na nilishawahi kucheza nao,” alisema Kaze.
Tambwe na Kaze wameingia mikataba ya miaka miwili na Simba wakitokea klabu ya Vital'O ya Burundi, ambayo wametoka kuipa ubingwa wa Kombe la Kagame Julai mwaka huu.
Tambwe alisema jana kuwa alisainia mkataba Julai 7 mwaka huu wakati Kaze alikiri pia kumwaga wino wa kuichezea Simba Agosti 7. Mikataba ya wawili hao na klabu ya Vital'O itamalizika Septemba 27, siku ya kufungwa kwa msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu ya Burundi.
ZIARA KAHAMA
Katika hatua nyingine, Tambwe na Kaze leo wanatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyanga kuungana na wachezaji wenzao wa Simba ili kujiandaa na mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara watakayocheza Jumamosi dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Katibu mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliiambia NIPASHE jana kuwa tayari wameanza taratibu za kuwatafutia nyota hao vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kama taratibu zinavyoelekeza.
Mtawala alisema kuwa leo wanatarajia kutuma dola za Marekani 5,000 (Sh. milioni 8) kwa viongozi wa klabu ya Vital'O ya Burundi ili kukamilisha uhamisho wao wa kimataifa (ITC).
Kuwasili kwa wachezaji hao juzi usiku kunaifanya idadi ya wachezaji wa kigeni wa Simba kuwa wanne, wakiwamo kipa Abel Dhaira na beki wa kati Joseph Owino.
Endapo Simba itashindwa kukamilisha uhamisho wa Warundi hao hadi kufikia kesho (Alhamisi), wachezaji hao watashindwa kuitumikia timu hiyo katika mechi yao dhidi ya Rhino.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: