CCM sasa yawaonya wanaoanza kuwapigia `debe` wanaofaa urais
Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa onyo kwa wanachama wake wakiwamo wabunge
ambao wameanza tabia ya kutangaza kuwa wangependa viongozi fulani
wagombee urais bila kufahamu kuwa kufanya hivyo kutaleta mgawanyiko
ndani ya Chama.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vPPS2T8q7zV-lKYYXbrn-lf5bdqJIcYFl7uEc4-ZgtU5jBGOD9tJlw3KTt07F1_G8fQ40GVLKU8oR0CvT9FkqrmsBi6T4NcT3wCMaS2DKZOVIssaNBHJ-Ymyurd7PYwQT2RQ7G=s0-d)
Naibu Katibu CCM Bara, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akijibu maswali kwa njia ya mtandao wa Facebook aliyokuwa akiulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusu hatua gani zimekuwa zikichukuliwa na chama hicho kwa wanachama walioanza kutangaza mapema kwamba wangependa kiongozi fulani awe mgombea urais 2015.
Nchemba alisema kila mara chama hicho kimekuwa kikiwakemea wanachama wanaotoa kauli zinazoweza kuleta mpasuko ndani ya Chama lakini bahati mbaya wamekuwa hawasikii.
“Tumeshakemea na tutaendelea kulikemea na kuwapa onyo kila mara,” alisema Nchemba.
Tamko hilo la CCM limekuja siku tano tu baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni mstaafu, John Komba, kuvunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye mwaka 2015.
Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kwa rais 2015.
Itakumbukwa Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM), naye alivunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Shelukindo alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.
Komba ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Kikwete ni Lowassa. Komba aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.
“Nakuambia Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais... unafikiri kuna mwingine. Nina sababu zangu tatu,” alisema Komba na kuhoji:
“Wewe unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia kwa fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo Lowassa?,” alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM kwenye kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.
Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatskuwa, Komba alisema: “Mimi sikwambii ni nani, lakini wapo mawaziri waliomkana, lakini leo hii wapo kwenye Serikali hii hii ya Rais Kikwete.
“Mimi nasema Lowassa na kama akipita sawa nitaburudiiika kwelikweli, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua, nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wana-CCM ule si wa Komba.” alisema.
Mbali na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na hata wananchi wanakikubali.
Akizungumzia suala la rushwa ndani ya CCM, Komba alisema kama Chama kuna watu wa aina nyingi, kuna wasafi, kuna wachafu lakini wote wako kwenye mstari mmoja.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: