Sengondo Mvungi apigwa mapanga
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, amelazwa katika
Kitengo cha Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa (Moi) kwenye
Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu
wanaoaminika kuwa ni vibaka.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uJZOjupWo-I-eUKePFekuxO9eDTuDUM6t23u3r0y_uKlfCa-FgG2gRu9OnNJ4ijhWiKshI9Xlxg1fIflzU3CcouVOweqNUVGc21HAKjfo6SdD8P_OkNGqwgYEFXNS7IOan-uAo6QyYDfjmaQhqLDN8=s0-d)
Dk. Mvungi, aliyewahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alipatwa na mkasa huo nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam saa 6:30 usiku wa kuamkia jana.
Vibaka hao wanaodaiwa walikuwa sita, walivamia nyumba ya D. Mvungi, ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya kisheria wa chama cha NCCR-Mageuzi, wakiwa na mapanga pamoja na baruti.
Taarifa za awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, zilieleza kuwa baada ya vibaka hao kuingia nyumbani kwa Dk. Mvungi, walimlazimisha mfanyakazi wake mmoja kueleza alipo (Dk. Mvungi).
Mbatia alisema baada ya kumlazimisha mfanyakazi huyo kwa kumpa kichapo, alilazimika kuongozana nao na kuwapeleka chumba alikokuwa amelala Dk. Mvungi.
Alisema kati ya vibaka hao, wanne waliongozana na mfanyakazi huyo na wawili walibaki nje na kabla ya kufika katika chumba cha Dk. Mvungi, waliobaki nje walilipua baruti.
Aidha, alisema mlio wa baruti hiyo ulimshitua Dk. Mvungi aliyekuwa amelala na ndipo alipotoka chumbani na kukutana na vibaka wanne ambao walimkata kwa panga utosini.
Alisema shambulio hilo lililamfanya Dk. Mvungi kuangukia paji la uso sakafuni na kutokwa na damu puani na masikioni.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, vibaka hao wanne waliingia chumbani na kumwambia mke wa Dk. Mvungi atoe fedha vinginevyo watamuua. Mbatia alifafanua kuwa mkewe Dk. Mvungi, aliwapa kiasi fulani cha fedha lakini vibaka hao hawakuridhika na kuanza kupekua kabatini ambako walifanikiwa kuchukua kompyuta mpakato moja (laptop) na bastola.
Alisema dereva wa Dk. Mvungi alipiga simu kwa majirani kwa ajili ya kutoa msaada ambao walifika na kumpeleka Hospitali ya Tumbi kupatiwa huduma ya kwanza ambako alishonwa nyuzi nne.
Kwa upande wake, mtoto wa kaka yake Dk. Mvungi, Deogratius Mwarabu, alisema baada ya kupewa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Tumbi, alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili saa 10:00 alfajiri kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha CT- Scan.
Mwarabu alisema tangu saa 10:00 alifajiri hadi saa 4:15 asubuhi, majeruhi huyo hakupewa huduma yoyote kwa kile kilichoelezwa kuwa mtaalam wa mashine ya CT-Scan hakuwapo kazini.
Alisema saa 4:15 asubuhi, Dk. Mvungi alitolewa Muhimbili na kupelekwa hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kufanyiwa kipimo hicho.
Aidha, alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi huo, alirudishwa tena Taasisi ya Mifupa (Moi), saa 5:15 asubuhi ambako amelazwa katika Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU).
"Hali ya baba siyo nzuri kwa kuwa hadi sasa damu zinatoka puani na masikioni na amepelekwa ICU," alisema Mwarabu.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia nyumbani kwa Dk. Mvungi usiku wa kuamkia jana na kumjeruhi vibaya.
"Siwezi kusema ni majambazi au vibaka ila ni watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamemvamia Dk. Mvungi na kumwibia laptop na bastola na tumeshaanza uchunguzi wa awali," alisema Kamanda Wambura.
Hata hivyo, alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo hadi jana.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: