Samatta aing`arisha TP Mazembe
Mshambuliaji
Mbwana Samatta wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo aliendeleza kasi yake ya kufunga katika kila mechi kwenye michuano
ya Kombe la Shirikisho wakati timu yake ikishinda 3-0 dhidi ya FUS
Rabat ya Morocco juzi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania alifunga goli la pili katika dakika ya 12 baada ya Mghana Solomon Asante kuwafungia bao la ufunguzi mabingwa hao wa Jamhuri ya Kongo.
Mabingwa hao wa zamani wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika walijihakikishia pointi tatu muhimu katika kundi lao la B wakati mchezaji wa kimataifa wa Mali, Cheibane Traore alipowafungia goli la tatu katika dakika ya 10 baada ya mapumziko.

Kocha wa Mazembe, Mfaransa Patrice Carteron alianza mechi hiyo kwa kupanga kikosi cha kushambulia zaidi ambapo licha ya wafungaji wa mabao yao, pia walikuwamo Tresor Mputu Mabi na Rainford Kalaba.
Samatta mwenye miaka 21, sasa amefikisha magoli manne katika michuano ya mwaka huu, akiwa amefunga pia katika mechi zote za nyumbani na ugenini dhidi ya Liga Muculmana ya Msumbiji baada ya Mazembe kuangukia kwenye michuano hiyo kufuatia kutolewa kwao katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Alifunga pia ugenini na kuisaidia Mazembe kuambulia sare ya 1-1 katika mechi yao dhidi ya Entente Setif ya Algeria.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: