PAMOJA NA KUMSAJILI FELLAINI,TATIZO KUBWA LA MANCHESTER UNITED NI KUTOKUWA NA MAWINGA MACHACHARI.……
Tangu enzi za kina George Best,David
Beckham, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs ambaye mpaka sasa anaendelea kuichezea
timu hiyo, Manchester Utd imekuwa ikisifika kwa kuwa na mawinga hodari.
Mapungufu makubwa ndani ya kikosi cha Manchester Utd kwa siku za karibuni ni kukosekana kwa mawinga hodari kama ilivyokuwa huko nyuma.
Kwa mtazamo wangu lingekuwa jambo la busara kama David Moyes
angemsajili walau winga mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa hapo jana.
Viwango vya mawinga wa Man Utd msimu
uliopita vilikuwaje?
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa
mawinga watatu wa klabu hiyo ; Ashley Young, Nani na Antonio Valencia:
michezo
|
magoli
|
Nafasi zilizotengenezwa
|
Pasi
|
|
Nani
|
11
|
1
|
11
|
2
|
Young
|
19
|
0
|
35
|
3
|
Valencia
|
30
|
1
|
40
|
5
|
Ukiangalia jedwali hapo juu utaona
mawinga wote watatu hawakuwa na makali mbele ya lango la timu pinzani,wachezaji
wote watatu kwa pamoja walichangia kwa 2.3% ya mabao yaliyofungwa na UNITED msimu
uliopita, inasikitisha mchezaji kama Ashley Young alishindwa kufunga walau bao
moja huku winga wa Sunderland Adam Johnson akifunga mabao matano.
Siyo tu wachezaji hawa walikuwa na
msimu mbaya kwenye sekta ya kupachika mabao,pia hawakuwa na mchango wa kutosha
kwenye sekta ya kusaidia wenzao kufunga
kwa pamoja wote watatu msimu uliopita walichangia 19.6% ya nafasi za mabao zilizotengenezwa na Manchester
United. Kwa upande mwingine wachezaji watatu wa Chelsea Oscar, Eden Hazard na
Juan Mata kwa pamoja walitengeneza 47% ya nafasi zilizotengenezwa na Chelsea
msimu uliopita.
Kiuhalisia Man Utd ilitegemea
mchango mkubwa kutoka kwa hawa mawinga kutokana na utamaduni wa klabu
kushambulia mara nyingi kupitia pembeni,kwa mantiki hiyo mawinga hawakuwa na
msaada msimu uliopita kutokana na takwimu zilizopo kitu kilichopelekea Sir Alex
Ferguson kulazimika wakati mwingine kumchezesha pembeni Danny Welbeck hasa
kwenye baadhi ya mechi kubwa,na hicho kilidhihilisha Ferguson kutokuwa na imani
kwa hao mawinga wake watatu.
Nini cha Kufanya?
Mazungumzo mengi ya wadau wa soka
hasa mashabiki wa Man Utd walikuwa wakisisitiza timu hiyo kumsajili kiungo wa
kati lakini sehemu ambayo kweli ilikuwa inahitaji marekebisho ya haraka ni
kwenye sehemu ya kiungo cha pembeni.
Nadhani walishaona hayo mapungufu ndio maana msimu uliopita
walipambana kweli kuwasajili Lucas Moura na Eden Hazard lakini mwisho wa siku
wachezaji hao walichagua kujiunga na vilabu vingine (labda ni kutokana na
wachezaji hao kuhitaji mishahara mikubwa ).
Kwasasa Ashley Young ana umri wa miaka
28 na kusema ukweli hajaonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge na Man Utd akitokea
Aston Villa, pamoja na msimu uliopita kukosa mechi kadhaa kutokana na majeraha
lakini bado hajaonyesha cheche zake.
Nani ni mchezaji mwenye kipaji
lakini amekuwa na kiwango cha kupanda na kushuka kama homa za vipindi tangia
ajiunge na Manchester United.
Valencia ni mchezaji mzuri lakini
hana rekodi nzuri ya kufunga mabao na kibaya zaidi ni winga pasee.lakini
amekuwa na msaada kwa staili yake ya uchezaji amekuwa akiisaidia sana timu kuwa
na balance kwenye upande wa kulia:
Ukiangalia jedwali hapo juu utaona
Valencia alivyo na mchango kutokana na aina ya uchezaji wake hasa pembeni kulia, amekuwa
akiisaidia timu kupanua uwanja hasa kipindi ambacho inahitaji huduma hiyo
pamoja na Valencia kuwa na msaada bado kutokana na aina yake ya kiuchezaji timu
haimuhitaji katika kila mchezo.
Uwajibikaji wake unamfanya kuwa na faida kwenye
timu kuliko wenzake kina Nani na Young mfano tu msimu uliopita takwimu
zinaonyesha alikuwa na msaada mkubwa kwenye ulinzi msimu
uliopita ambapo79% ya tackles zake
alifanikiwa kuipata mipira kutoka kwa wachezaji wa timu pinzani,Kwa Valencia huu ulikuwa mchango mkubwa kwa timu hasa
kwa jukumu lake akiwa kama winga.
Hitimisho.
Mawinga
wa Manchester United wana
udhaifu ukilinganisha na idara zingine ndani ya kikosi kitu
kilichopelekea
wachezaji kama Shinji Kagawa na Danny Welbeck kulazimishwa kucheza
pembeni. Ashley Young na Luis Nani wanatakiwa kuongeza viwango vyao
ingawa kuna
kijana mpya Wilfred Zaha amabaye bado hana uzoefu.
Pamoja na Machester Utd kumsajili
kiungo hodari Maroune Fellaini lakini mapungufu makubwa waliyokuwa nayo kwasasa ni kuwakosa mawinga machachari.
0 comments: