Mwanamke jambazi apigwa kichwa akijaribu kupora M-Pesa kwa bastola

Jaribio la kupora fedha katika kituo cha M-Pesa lililofanywa na Anita Kaburu (27),  pamoja na mwenzake wakitumia bastola na bunduki, lilishindikana baada ya mteja mmoja kumpiga kichwa na kufanikiwa kumdhibiti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa Anita ambaye ni mkazi wa Usa River wilayani Arumeru, alivamia kituo cha M-Pesa kinachomilikiwa na Stela Mrema akiwa na mwanamume mmoja.

Alisema watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi, baada ya kufika kwenye kituo cha huduma hiyo maeneo ya Shamsi jijini hapa majira ya saa 6:00 mchana wakijifanya wateja,  ghafla mmoja wao (Anita) alichomoa bastola kwenye mkoba wake na mwenzake akatoa bunduki na kuamrisha wapewe fedha.

“Baada ya kuingia walijifanya kuhitaji huduma ya M-Pesa, ghafla yule mwanamke alitoa bastola kwenye mkoba wake na mwanaume naye alitoa bunduki na kuwaamuru watoe pesa na simu… ndipo yule mteja alimpiga kichwa yule mwanamke na kisha kupiga kelele za kuomba msaada hivyo walifanikiwa kumdhibiti,” alisema.

Hata hivyo, alisema mwenzake alifanikiwa kukimbia. Alisema baada ya polisi kumtaka Anita awataje wenzake, polisi waliwakamata watuhumiwa wanne waliokuwa wamepanga kufanya uporaji huo.

Kamanda Sabas aliwataja waliokamatwa kuwa ni Abdulahman Jumanne Idd (27) ambaye ni mwangalizi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK na mkazi wa Shamsi, Simon Martine au Mapanki (45) mkazi wa Kwa Mrombo, Hashimu Ally (30) ambaye ni mpanda milima na mkazi wa Ngarenaro na Charles Luangano (24) ambaye pia ni mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya KK.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kufanyiwa upekuzi walikamatwa na bunduki aina ya shotgun, bastola aina ya bereta na risasi sita za bastola. Alisema watafikishwa mahakamani Jumatatu.

0 comments:

Anthery Mushi azikwa bila huduma ya kikanisa

Familia ya Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi Jumapili iliyopita baada ya kumuua kwa risasi mkwewe, Anastazia Saro, amezikwa bila huduma ya kikanisa kijijini kwao Ongoma.

Kanisa Katoliki, Parokia ya Uru ilishindwa kutoa huduma hiyo kutokana na mazingira ya kifo chake.

Licha ya hali hiyo kujitokeza, familia hiyo, ilionyesha nia yake ya kwenda kumuangukia Paroko wa Parokia wa Kanisa hilo, ili aridhie familia ya Anthery, isome misa maalumu ya kuomba ndugu yao afutiwe dhambi inayomkabili.

Mushi (40), alijipiga risasi baada ya kumuua mkwewe na kumjeruhi mzazi mwenziwe Ufoo Saro, mtanzangazi wa kituo cha televisheni cha ITV,  eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Wakati familia ya Mushi ikiazimia hilo, kiongozi aliyeteuliwa na familia kufanya ibada ya maziko, baba mdogo wa Mushi, Ugolin Mushi alisema kuwa Watanzania wanapaswa kutomhukumu kwa alichokitenda na kwamba imetosha kwa kuwa kinachoelezwa kila kona ya nchi baada ya tukio hilo ni sawa na mbu kubadilika na kuwa tembo.

“Sisi ni nani hadi tumhoji Mwenyezi Mungu juu ya kilichotokea maana mbu anaweza kubadilika na kuwa mkubwa kama tembo kutokana na habari zinazotangazwa.

Anayejua ukweli huu ni Anthery na Mungu wake…Lakini Mungu amsamehe makosa yake wakati wa vita na wakati wa amani, wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa na akafurahi na malaika huko aendako,” alisema.


Hata hivyo, mtoto wa marehemu, Alvin Anthery, ambaye amezaa na Ufoo, hakuweza kumzika baba yake kutokana na sababu zisizojulikana.

Hali ilikuwa tulivu nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Ongoma, Uru Kaskazini, tofauti na matarajio ya wengi baada ya kuwasili kwa mwili huo usiku wa kuamkia jana, ingawa mamia ya wakazi wa Uru walifurika kushuhudia mazishi ya Anthery ambaye  amelitikisa taifa kwa siku kadhaa kutokana na tukio la mauaji Oktoba 13, kugonga vichwa vya habari.

Juzi, familia ya Anthery, ilinukuliwa wakati wa kuuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), ikiliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kutokana na ndugu yao kukutwa na risasi mbili.

Mwili wake baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ulikutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.

Licha ya kanisa kutotoa huduma ya ibada ya mazishi ya Anthery, watawa wa kanisa waliohudhuria katika msiba huo walishindwa kuendesha ibada kutokana na taratibu za kanisa.

0 comments:

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA: MWANDISHI WA ITV APIGWA RISASI.

Mtu 1 amempiga risasi na kumjeruhi mwandishi wa ITV/radio One Ufoo Saro,kisha kumpiga risasi na kumuua papo hapo mama yake mzazi Ufoo,na baadaye yeye mwenye kujiua baada ya kutekeleza adhama yake hiyo huko Kibamba jijini DSM.

0 comments:

Mkapa atoa siri kufeli kidato cha nne

Rais Mstaafu Benjamini Mkapa amesema kuwa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana kulichangiwa na mazingira mabovu ya kujifunzia, wanafunzi kutokupenda kujisomea pamoja na uhaba wa vifaa
.

Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozindua mpango wa usomaji vitabu wenye lengo la
Learn more »

0 comments:

katika picha;jezi mpya ya Brazil katika kombe la dunia

0 comments:

Mfanyabiashara amwagiwa tindikali Arusha

Mfanyabiashara wa madirisha ya alluminium jijini Arusha, Japhet  Minja (30), amelazwa katika Hospitali ya Selian jijini hapa, baada ya kumwagiwa kimiminika kinachodaiwa kuwa ni tindikali usoni na watu wasiojulikana
.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa 12:15 alfajiri katika eneo la Shamsi, wakati
Learn more »

0 comments:

Mangula: Najuta kuishi jimbo la Halima Mdee

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi kwao.

Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za 
Learn more »

0 comments:

Serikali kuziongezea mikopo sekta binafsi

Serikali imesema itaendelea kuziwezesha sekta binafsi nchini ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 na kuchagiza ukuaji wa haraka wa uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu ushiriki wa sekta binafsi
Learn more »

0 comments:

Lema fupa gumu

  Serikali sasa yaondoa kesi dhidi yake kortini
  Ni ile polisi walioruka ukuta usiku kumkamata
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kufanya uchochezi kwa wanafunzi wa Chuo cha
Learn more »

0 comments:

Serikali yayajia juu MWANANCHI, Rai

Serikali imesema imebaini kuwa baada ya gazeti la Mwananchi kufungiwa, limeendelea kuchapishwa kwenye mtandao wa internet, hivyo imeutaka uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kuacha kufanya hivyo mara moja, vinginevyo italifungia katika muda usiojulikana au italifuta kabisa.

Mbali na kuutaka uongozi wa MCL kufanya hivyo, pia imeutaka uongozi wa Kampuni ya New
Learn more »

0 comments:

Sheikh Ponda akwaa kisiki

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro, imetupilia mbali ombi liliwasilishwa na upande wa utetezi wa kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh   Ponda Issa Ponda, la kuitaka kumfutia shtaka la kwanza au kulihamishia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ikisema zote zina mamlaka sawa kisheria.

Learn more »

0 comments:

Chikawe afichua siri nzito muswada Katiba mpya

  Ataja vifungu sita vilichomekwa
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe
Serikali imekiri kuwa vifungu sita katika muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba vilivyoongezwa na kuwasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopita, havikupelekwa Zanzibar kutolewa maoni.
Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.

Learn more »

0 comments:

Maandamano yatikisa Dodoma

Maelfu ya wakazi wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani katika Manispaa ya Dodoma, wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.


Wakazi hao waliandamana jana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya Manispaa ya Dodoma wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, kuzungumza nao ili kuwaeleza hatima ya nyumba zao 1,000 kubomolewa kwa madai ya kulivamia eneo la CDA.

Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe mbalimbali wakupinga hatua hiyo.

Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo mbalimbali huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama “CDA ni zaidi ya al Shaabab”, “CCM mnaiona bomoabomoa”, “CDA ni zaidi ya Nduli Idd Amini Dada” na lingine likisomeka “hata wanyama hupewa hifadhi.”

Wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri Dk. Nchimbi, baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.

Andrew Mdumi, mMenyekiti wa Mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa, alisema waliamua kufanya maandamano hayo baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.

Mdumi alisema kuwa CDA imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kuwaahidi kuwa wataalamu wake wa ardhi watakwenda kuwapimia, lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kuanzia Septemba 23, mwaka huu kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya bustani za mbogamboga na matunda.

“Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda, hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi, kuna nyumba zaidi ya 1,000 ambazo wanataka kuzibomoa kwa ajili tu ya kupisha bustani,” alisema.

Alisema wakazi hao wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo kwa gharama zao wenyewe.

Mwenyekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu Kusini, Mathew Ndallu, alisema kuwa katika kufuatilia kupimiwa viwanja, walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waende kufanya utambuzi wa nyumba zilizopo Mapagale na Misingi ili ufanyike upimaji.

 Ndallu alisema walikubaliana kuwa kwa eneo hilo kuwa halijapimwa, wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.

“Tulikubaliana nao baada ya wao (CDA) kuja kutambua idadi ya nyumba Mapagale na Misingi watupimie na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha Shilingi 500,000 kwa kila mwenye eneo,” alisema Ndalllu.

 Aliongeza kuwa baada ya CDA kuonekana kutoridhika na kiasi hicho, wananchi  walisema watakuwa tayari kuongeza Sh. 200,000 ili gharama za kupimiwa zifikie Sh. 700,000.

Hata hivyo, alisema katika hali ya kushangaza wakati wakisubiri kupimiwa, CDA iliwageuka na kuwataka kwanza wapatiwe viwanja 500 ili wawapimie.

“Mara baada ya kukubaliana nao kuwa tuko tayari kuchangia, Mkurugenzi alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili waje kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea,” alisema Ndallu.

Alisema baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo, aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya jana ili leo zoezi la kubomoa nyumba zao lianze.

“Walituandikia barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
 Alisema kutokana na CDA kushindwa kusikiliza kilio chao, wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao.

Alisema kuwa jumla ya mitaa minne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi na Image A na B.

RC ATENGUA AMRI
Akizungumza na kundi la wakazi hao, Dk. Nchimbi alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika kwa ajili ya mazungumzo ya kupata mwafaka.

“Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kufikia mwafaka kwani kubomoa siyo suluhu, hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya suala hili,” alisema Dk. Nchimbi na kuongeza:

“Mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazitawaumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.”

Baada ya Mkuu wa mkoa kutamka kutengua amri hiyo, wananchi hao walipaza sauti kwa furaha huku wengine wakisema wanamuombea kiongozi huyo miaka 20 zaidi ya uongozi kama mkuu wa mkoa na ikiwezekana astaafie kazi mkoani Dodoma.

CDA: BOMOABOMOA PALE PALE
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskas Muragili, hata hivyo, baadaye aliliambia NIPASHE kuwa  agizo la mkuu wa mkoa hajalipata kimaandishi, hivyo zoezi la kubomoa nyumba hizo liko pale pale kwa kuwa CDA ilishatoa notisi ya siku saba kwa wamiliki wa nyumba hizo kuzibomoa wenyewe.
Alisema kuwa CDA ni mamlaka inayojisimamia na kuongozwa na sheria.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Maalim Seif ataka Zanzibar huru

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, amesema mgogoro wa Muungano uliopo unatokana na kufichwa kwa makubaliano yaliyowekwa na waasisi wa Muungano  na kwamba  kero hizo hazitokwisha hadi kuwapo kwa Serikali tatu na Muungano wa mkataba.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu  Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyasema hayo juzi wakati wa Kongamano la Wazanzibari waishio Tanzania Bara na kusema kuwa Muungano uliotiwa saini na waasisi wa Muungano huo umefichwa na hivyo kusema dawa yake ni kuwapo kwa Serikali tatu na  Muungano wa mkataba.

Maaalim Seif  alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013 kwa maelezo kuwa una kasoro.

“Wazanzibar wenzangu, mimi pia ni mmoja wa Wazanzibar ambao tunataka Muungano wa mkataba… nilipoulizwa na tume nilisema nataka Muungano wa mkataba… nadhani nanyi pia mawazo yenu ni kama mimi,” alisema.

Hata hivyo, aliisifu Serikali ya Rais Kikwete kwa kuwaachia wananchi wenyewe kuiandika Katiba yao, lakini  alimtahadharisha kutokuwa na wazo la kutia saini Muswada huo.

Alisema Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kama ilivyo kwa nchi nyingine, hivyo inahitaji kurejeshewa mamlaka yake na kuwa na maamuzi ikiwa na pamoja kurejeshewa kiti chake katika Baraza la Umoja wa Kimataifa (UN).
Learn more »

0 comments:

Mwandishi amuokoa Mkenya wa Dk. Ulimboka kwenda jela

Raia wa Kenya, Joshua Muhindi, aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la kutoa maelezo
Learn more »

0 comments:

Mahakama kuamua ombi la Sheikh Ponda leo

Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, inatarajiwa kusikilizwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro na kutolewa  uamuzi wa ama kumfutia shtaka la kwanza linalomkabili au kulihamisha katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Learn more »

0 comments: